Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abdelkarim Hussein Mohamed al-Nasser

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Juni 25 mwaka 1996, wanachama wa Saudi Hizballah walifanya mashambulizi ya ugaidi kwenye jengo la Khobar Towers karibu na Dhahran, Saudi Arabia. Muda huo jengo hilo lilikua likitumika kama makazi ya wafanyakazi wa jeshi la Marekani. Magaidi waliendesha gari la kubebea mafuta lililojazwa milipuko kwenye maegesho ya gari na kulilipua, wakiharibu jengo la jirani. Shambulizi liliua wanajeshi 19 wa Marekani na raia mmoja wa Saudi, na kujeruhi 372 wa mataifa mengine mbalimbali.

Mtu aliyeorodheshwa hapo juu ameshtakiwa katika mahakama ya Wilaya ya Mashariki ya Virginia Juni 25, 1996, kwa kulipua bomu jengo la Khobar Towers huko Dharran, Saudi Arabia.

Mtu aliyetajwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:

Njama ya kuwaua raia wa Marekani, njama ya kufanya mauaji, njama ya kutumia silaha za maangamizi dhidi ya raia wa Marekani, njama za kuharibu mali za Marekani. Njama ya kushambulia huduma za ulinzi wa kimataifa, kulipua mabomu na kusababisha vifo, kutumia silaha za uharibifu mkubwa dhidi ya raia wa Marekani, mauaji kwa kutumia mbinu za uharibifu wakati wa uhalifu, Mauaji ya wafanyakazi wa serikali, na kujaribu kuua wafanyakazi wa serikali.