Tafutwa
Taarifa ambayo inaleta haki...

Abdelbasit Alhaj Alhassan Haj Hamad

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Mnamo Januari 1, 2008, raia wa Marekani na mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Kimataifa (USAID) John Granville na dereva wake raia wa Sudan, Abdelrahman Abbas Rahama, walipigwa risasi na kufariki dunia wakiwa njiani kuelekea nyumbani kwao wakitokea kwenye mkesha wa kuuaga mwaka mjini Khartoum, Sudan.  Granville mwenye umri wa miaka 33, alikuwa anafanya kazi kuhusu demokrasia na utawala bora nchini Sudan.  Abbas, mwenye umri wa miaka 39, alijiunga na USAID mnamo mwaka 2004 kama mjumbe wao wa Timu ya Majanga na Usaidiaji kwa mji wa Darful.  Makundi mawili kwa nyakati tofauti yalijitangaza na kutamba kuwa ni wahusika wa shambulio la mauaji. Ansar al-Tawhid (Waunga mkono wa itikadi yauwepo wa Mungu mmoja pekee – Monotheism) na al-Qaida katika Ardhi ya Mito Miwili ya Nile (AQTN).

Mfumo wa sheria wa Sudan uliwashitaki na kuwafunga watu watano kwa ushiriki wao katika mauaji.  Abdelraouf Abu Zaid Mohamed Hamza, Mohamed Makawi Ibrahim Mohamed, Abdelbasit Alhaj Alhassan Haj Hamad, na Mohanad Osman Yousif Mohamed walihukumiwa kifo kwa cha kunyongwa, lakini walitoroka gerezani mwaka mmoja baada ya hukumu yao.  Mohanad aliripotiwa kufariki huko Somalia mnamo Mei 2011.  Abdelraouf alikamatwa na mamlaka ya Sudan. Makawi na Abdelbasit bado hawajakamatwa na kutiwa nguvuni.

Abdelbasit alikuwa mpiga risasi wa pili katika gereza la Khobar lililopo mjini Khartoum mnamo Juni 11, 2010, na sasahivi yupo Somalia.