Habazi mpya za sasa

Qasim al-Rimi

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 10

Qasim al-Rimi aliitwa jina la emir wa AQAP mnamo mwezi Juni 2015, mara baada ya kuapa utii kwa kiongozi wa al-Qaida Ayman al-Zawahiri na kutoa wito wa mashambulizi mapya dhidi ya Marekani. Al-Rimi aliwafundisha magaidi kwenye kambi ya al-Qaida huko Afghanistan miaka ya 1990, kisha akarejea Yemen na akawa Kamanda wa kijeshi wa AQAP. Alihukumiwa miaka mitano gerezani ndani ya Yemen mnamo mwaka 2005 kwa kupanga njama ya kumuua Balozi wa Marekani wa Yemen, na alitoroka mwaka 2006. Al-Rimi amehusishwa na shambulio la Septemba 2008 katika Ubalozi wa Marekani huko Sana’a ambao uliacha walinzi 10 wa Yemen, raia wanne, na magaidi sita wamekufa. Al-Rimi pia alihusishwa na jaribio la 2009 la bomu la kujitoa mhanga la “mlipuaji wa bomu wa chupi” Umar Farouq Abdulmutallab ndani ya ndege iliyokuwa inaelekea Marekani. Mnamo 2009, serikali ya Yemen ilimtuhumu kuwa anaendesha kambi ya mafunzo ya al-Qaida katika jimbo la Abyan la Yemen.

(Habari yote (habari kamil) »)

Khalid Saeed al-Batarfi

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Khalid al-Batarfi ni mwanachama mwandamizi wa AQAP katika Gavana ya Hadramaut Yemen na aliyekuwa mwanachama wa Baraza la AQAP la shura. Mwaka 1999, alisafiri hadi Afghanistan, ambapo alifundishwa katika kambi ya al-Qa’ida al-Farouq.Mnamo 2001, alipigana pamoja na Watalebani dhidi ya vikosi vya Marekani na Umoja wa Kaskazini. Mwaka 2010, al-Batarfi alijiunga na AQAP huko Yemen, aliongoza wapiganaji wa AQAP katika kuchukua Wilaya ya Abyan ya Yemen, na aliitwa jina la AQAP emir wa Abyan. Kufuatia kifo cha kiongozi wa AQAP, Nasir al-Wuhayshi katika shambulio la kijeshi la Marekani la mnamo Juni 2016, alitoa taarifa ya onyo kuwa al-Qaida wataharibu uchumi wa Marekani na kushambulia maslahi mengine ya Marekani.

(Habari yote (habari kamil) »)

Abdullah Ahmed Abdullah

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 10

p>Abdullah ni kiongozi wa ngazi za juu wa al-Qa’ida na mwanachama wa Baraza la uongozi wa al-Qa’ida, ya “majlis al-shura.” Abdullah ni ofisa mshikafedha mwenye uzoefu, mwezeshaji, na mpangaji wa uendeshaji wa al-Qa’ida.

Abdullah alihukumiwa na kushtakiwa na shirikisho la baraza kuu mnamo Novemba 1998 kwa jukumu lake la mabomu katika Ubalozi wa Marekani ndani ya Dar-es-Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya mnamo Agosti 7, 1998. Mashambulizi yaliua raia 224 na kujeruhi wengine zaidi ya 5,000.

Katika mwaka 1990, Abdullah alitoa mafunzo ya kijeshi kwa wafanyakazi wa al-Qa’ida na wanaume wa makabila wa Somalia ambao walipigana dhidi ya vikosi vya Marekani huko Mogadishu wakati wa operesheni ya kurejesha matumaini. Kutoka mwaka 1996-1998, yeye aliendesha kambi nyingi za mafunzo ya al-Qa’ida ndani ya Afghanistan.

(Habari yote (habari kamil) »)

Sayf al-Adl

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 10

Al-Adl ni kiongozi mwandamizi wa al-Qaida na mwanachama wa baraza la uongozi wa AQ, “majlis al-shura.” Al-Adl pia anaongoza kamati ya kijeshi ya al-Qaida.

Al-Adl alihukumiwa na kushtakiwa na shirikisho la baraza kuu mnamo Novemba 1998 kwa jukumu lake la mabomu katika Ubalozi wa Marekani ndani ya Dar-es-Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya mnamo Agosti 7, 1998. Mashambulizi yaliua raia 224 na kujeruhi wengine zaidi ya 5,000.

Alikuwa luteni Kanali katika Mamlaka Maalum ya Misri mpaka kukamatwa mwaka 1987 na maelfu ya wapiganaji wengine wa kupambana na serikali baada ya jaribio la mauaji ya waziri wa mambo ya ndani wa Misri

(Habari yote (habari kamil) »)

Abdul Wali

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Abdul Wali ni kiongozi wa Jamaat ul-Ahrar (JuA), kikundi cha wanamgambo wenye mafungamano na Tehrik-e-Taliban Pakistan (TTP). Yeye aliripotiwa anafanya kazi kutoka majimbo ya Nangarhar na Kunar Afghanistani.

Chini ya uongozi wa Wali, JuA imekuwa moja ya mitandao ya operesheni ya inayofanya kazi zaidi ya TTP katika jimbo la Punjab na imedai kuhusika na mabomu ya kujitoa muhanga na mashambulio mengine kote Pakistani.

Katika Machi 2016, JuA iliofanya shambulio la kujitoa muhanga katika hifadhi ya umma katika Lahore, Pakistan ambalo liliua watu 75 na kujeruhi 340.

(Habari yote (habari kamil) »)

Mangal Bagh

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Mangal Bagh ni kiongozi wa Lashkar-e-Islam, kikundi cha wanamgambo wenye mafungamano na Tehrik-e-Taliban Pakistan (TTP). Kundi lake linapata mapato kutoka biashara ya madawa ya kulevya, magendo, utekaji nyara, mashambulizi ya misafara ya NATO, na kodi kwenye biashara ya usafiri kati ya Pakistani na Afghanistani.

Bagh ameongoza Lashkar-e-Islam tangu mwaka 2006 na mara kwa mara kubadilisha Muungano ili kulinda mapato haramu wakati akitekeleza toleo la kali la Uislamu la Deobandi katika maeneo ya Afghanistan Mashariki na magharibi mwa Pakistani ambayo yeye udhibiti, hasa Mkoa wa Nangarhar, Afghanistani.

Alizaliwa katika Shirika la Khyber, Pakistani, inaaminika kuwa na umri katikati ya miaka arobaini. Bagh ni mwanachama wa kabila la Afridi. Alisoma katika madrasa kwa miaka kadhaa na baadaye kupigana sambamba na vikundi vya wanamgambo vya Afghanistan.

(Habari yote (habari kamil) »)

Ahlam Ahmad al-Tamimi

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Raia wa Jordan, Ahlam Ahmad al-Tamimi, pia anajulikana kama “Khalti” na “Halati,” ni gaidi mwendeshaji wa HAMAS aliyehukumiwa.

Mnamo Agosti 9, 2001, al-Tamimi alisafirisha bomu na mtoa mhanga wa bomu wa HAMAS kwenda Yerusalemu Sbarro pizzeria iliyojaa watu wengi, ambako mshambuliaji alilipua mabomu, na kuua watu 15, ikiwa ni pamoja na watoto saba. Raia wawili wa Marekani waliuawa katika shambulio – Judith Shoshana Greenbaum, mwalimu mjamzito mwenye umri wa miaka 31 kutoka New Jersey, na Malka Chana Roth, mwenye umri wa miaka 15. Wengine zaidi ya 120 walijeruhiwa, ikiwa ni pamoja na Wamarekani wanne. HAMAS walidai kuhusika na mabomu.

(Habari yote (habari kamil) »)

Talal Hamiyah

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 7

Talal Hamiyah ndiye mkuu wa Shirika la Usalama wa Nje wa Hizballah (ESO), ambalo linaweka seli zilizopangwa duniani kote. ESO ni kipengele cha hizballah kinachohusika na kupanga, kuratibu, na utekelezaji wa mashambulizi ya kigaidi nje ya Lebanoni. Mashambulizi hayo yamekuwa yanalenga Waisraeli na Wamarekani.

Idara ya Hazina ya Umoja Kimarekaniilimtambua Talal Hamiyah mnamo Septemba 13, 2012 kama Mtawala Mkuu wa Kimataifa (SDGT) kwa mujibu wa Oda 13224 kwa kutoa msaada kwa shughuli za kigaidi za Hizballah huko Mashariki ya Kati na duniani kote.

(Habari yote (habari kamil) »)

Fuad Shukr

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Fuad Shukr ni mshauri mwandamizi wa muda mrefu juu ya mambo ya kijeshi kwa Katibu Mkuu wa Hizballah Hasan Nasrallah. Shukr ni mwandamizi wa Hizballah ambaye ni kamanda wa kijeshi wa vikosi vya Hizballah kusini mwa Lebanoni. Yeye hutumika kwenye bodi ya juu ya kijeshi ya Hizballah, Baraza la jihadi.

Shughuli za Shukr kwa niaba ya Hizballah zimechukua muda wa miaka 30. Alikuwa mshirika wa karibu wa kamanda wa Hizballah ambaye sasa amekufa Imad Mughniyah. Shukr alicheza jukumu kuu katika kupanga na kutekelezwa kwa mabomu ya Umoja wa Mataifa ya Oktoba 23, 1983 ya Marine Corps huko Beirut, Lebanoni, ambayo iliwaua wafanyakazi wa huduma 241 wa U.S

(Habari yote (habari kamil) »)

Muhammad al-Jawlani

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 10

Muhammad al-Jawlani, pia anajulikana kama Abu Muhammad al-Golani, pia anajulikana kama Muhammad al-Julani, ni kiongozi mwandamizi wa shirika la kigaidi, al-Nusrah Front (ANF), tawi la Syria la al-Qaida. Mwezi Aprili 2013, al-Jawlani aliahidi utii kwa al-Qaida na kiongozi wake Ayman al-Zawahiri. Katika Julai 2016, al-Jawlani alisifia al-Qaida na al-Zawahiri katika video ya mtandaoni na kudai ANF inabadilisha jina lake kwenda Jabhat Fath Al Sham ( “Ushindi wa Levant Front”). Chini ya uongozi wa al-Jawlani , ANF imefanya mashambulizi kadhaa ya kigaidi katika Syria, mara nyingi ikilenga raia. Mwezi Aprili 2015, ANF iliripoti utekaji nyara, na baadaye iliwaachilia, takriban raia 300 wa Kikurdi kutoka eneo la kituo cha ukaguzi katika Syria. Katika Juni 2015, ANF ilidai kuhusika na mauaji ya wakazi 20 katika kijiji Druze Qalb Lawzeh ndani ya jimbo la Idlib, Syria. (Habari yote (habari kamil) »)

Mauaji ya Joel Wesley Shrum

Taizz, Yemen | Machi 18, 2012

Machi 18, 2012, Shrum, mwenye umri wa miaka 29, alipigwa risasi na kuuawa akiwa njiani kuelekea kazini Taizz, Yemen, na mwenye bunduki aliyekuwa akiendeshwa nyuma ya pikipiki iliyosimama kando ya gari lake. Wakati wa kifo chake, Shrum alifanya kazi katika kituo cha maendeleo na Mafunzo cha kimataifa kama msimamizi na mwalimu wa Kiingereza. Alikuwa akiishi Yemen na mke wake na watoto wadogo wawili. Siku chache baada ya shambulio hilo, shirika la kigaidi la al-Qaida katika Peninsula ya Arabia (AQAP) walidai kuhusika na mauaji hayo. Programu ya zawadi ya haki ya Idara ya Marekani inatoa ofa ya zawadi ya hadi dola milioni 5 kwa habari zitakazopelekea kukamatwa au kushtakiwa kwa wale watu waliofanya, kupanga, au kusaidia katika mauaji ya raia wa Marekani Joel Shrum. (Habari yote (habari kamil) »)

Abu Bakr al-Baghdadi

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 25

Abu Bakr al-Baghdadi, anayejulikana pia kama Abu Du’a, pia anajulikana kama Ibrahim ‘Awwad Ibrahim Ali al-Badri, ni kiongozi mwandamizi wa kundi la kigaidi la Islamic State of Iraq na Levant (ISIL).Tishio ambalo al-Baghdadi analeta limeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu Idara ya nchi ilipotoa ofa ya awali ya dola 10 kwa ajili ya kutoa taarifa za kupelekea eneo lake, kukamatwa, au kushitakiwa ilitangazwa mwaka 2011. Katika Juni 2014, ISIL (pia inajulikana kama Da’esh) walichukua umiliki wa sehemu ya Syria na Iraq, alitangaza kuanzishwa kwa ukhalifa wa Kiislamu, na kumpa jina al-Baghdadi kama Khalifa. Katika miaka ya karibuni, ISIL imepata uaminifu wa makundi wanajihadi na watu wenye siasa kali duniani kote, na iliongoza mashambulizi nchini Marekani. (Habari yote (habari kamil) »)

Gulmurod Khalimov

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 3

Aliyekuwa kanali wa kikosi cha ukomandoo cha Tajikistan, kamanda wa polisi, na snaipa wa jeshi Gulmurod Khalimov ni mwanachama wa Dola ya Kiislamu ya Iraq na Levant (ISIL) na mshawishi wa wanachama wapya kujiunga. Yeye alikuwa ni kamanda wa wa kikosi maalumu cha kijeshi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tajikistan. Khalimov aliotokea kwenye video ya kipropaganda kuthibitisha kwamba anapigana tokea ISIL na akatoa wito wa wazi wa vitendo vya kihalifu dhidi ya Wamarekani. (Habari yote (habari kamil) »)

Abu-Muhammad al-Shimali

Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5

Mwandamizi wa juu wa serikali ya Kiislamu ya Iraq na Levant (ISIL) Mkuu wa mpaka Tirad al-Jarba, anayejulikana zaidi kama Abu-Muhammad al-Shimali, amekua akijihusisha na ISIL, zamani ikijulikana kama al-Qaeda nchini Iraq, tangu mwaka 2005. Sasa anatumika kama ofisa muhimu katika kamati ya Uhamiaji na Vifaa (usafirishaji), na anahusika na ufanikishaji wa usafiri wa (Habari yote (habari kamil) »)

Usafirishaji wa mafuta na mambo ya kale kulinufaisha Taifa la Kiislamu la Iraq na Levant (ISIL)

Mpango wa Tuzo za Haki unatoa zawadi nono hadi kufikia dola milioni 5 kwa taarifa inayopelekea uzuizi mkubwa wa mauzo na/au biashara ya mafuta na mabo ya kale ufanywao na, kwa au kwa niaba kunufaisha kikundi cha kigaidi cha Dola ya Kiislam ya Iraq na Levant (ISIL), ambalo pia hufaamika kwa kifupi chake kwa Kiarabu kama DAESH. (Habari yote (habari kamil) »)