Shirika la Ulinzi la Mapinduzi ya Kiislamu-Kikosi cha Qods(IRGC-QF), tawi la IRGC, ni utaratibu wa kimsingi ya nchi ya Irani kukuza na kuunga mkono makundi ya kigaidi nje ya nchi. Irani hutumia IRGC-QF kutekeleza malengo yake ya sera ya nje, kuficha harakati za kijasusi, na kuzua machafuko Mashariki ya Kati. Mnamo mwaka 2011, IRGC-QF ilipanga njama kumuua Balozi wa Saudia Marekani, jijini Washington D.C. Mnamo mwaka 2012, majasusi wa IRGC-QF walikamatwa nchini Uturuki na Kenya kwa kupanga mashambulio. Mnamo Januari mwaka 2018, Ujerumani ilifichua majasusi 10 wa IRGC waliohusika na njama ya kigaidi nchini Ujerumani.
Mnamo tarehe 15 mwezi Aprili, mwaka 2019, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja IRGC, kikiwemo kikosi cha IRGC-QF, kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Mnamo mwaka 2017, Wizara ya Fedha ya Makerani iliitaja IRGC kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa, kwa shughuli zake katika kuiunga mkono IRGC-QF. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya IRGC katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na IRGC. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa IRGC.