Shirika la Ulinzi la Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), sehemu ya jeshi rasmi la Irani, linatekeleza jukumu kuu katika matumizi ya Irani ya ugaidi kama chombo muhimu usimamizi wake stadi wa masuala ya serikali. IRGC hupanga, huratibu, na hutekeleza ugaidi kote duniani. Aidha, IRGC imeanzisha, ikaunga mkono na kuelekeza makundi mengine ya kigaidi. IRGC imehusika na mashambulio mengi yaliyowalenga Wamarekani na vifaa vya Marekani, yakiwemo yale ambayo yamewaua raia wa Marekani. Tangu iliopoanzishwa mnamo mwaka 1979, IRGC imepata jukumu kubwa katika kutekeleza sera ya nje ya irani. Kundi hilo sasa lina udhibiti katika sehemu kubwa za uchumi wa Irani na lina ushawishi katika siasa za ndani za Irani.
Mnamo tarehe 15 mwezi Aprili, mwaka 2019, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja IRGC, kikiwemo kikosi cha IRGC-Qods Force, kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Mnamo mwaka 2017, Wizara ya Fedha ya Makerani iliitaja IRGC kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa, kwa shughuli zake za kuunga mkono IRGC-QF. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya IRGC katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na IRGC. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa IRGC.