Shirika la Abu Nidal (ANO) liliundwa mnamo mwaka 1974 baada ya kujitenga kutoka Shirika la Uhuru wa Palestina. ANO lilihimiza kuangamizwa kwa israel na lilinuia kuvuruga juhudi za kidiplomasia zilizounga mkono mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati. Shirika hilo lilihusika na mashambulizi mengi ya kigaidi, likiwamo lile la bomu la ndege ya TWA Flight 840 (kiungo) na kutekwa nyara kwa Ndege ya Pan Am 73.
Mnamo tarehe 8, mwezi Oktoba, mwaka 1997, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza ANO kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni(FTO) chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Mnamo tarehe mosi, mwezi Juni, mwaka 2017, Wizara ya Mambo ya Nje ilibatilisha kutangazwa kwa ANO kama FTO.