Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu shambulio la bomu la mwaka 1996 dhidi ya majengo ya Khobar Towers karibu na Dhahran, Saudia. Mnamo tarehe 25 mwezi Juni, mwaka 1996, wanachama wa Saudi Hizballah walilipua lori la kubebea mafuta lililokuwa na vilipukaji vya plastiki kwenye eneo la maegesho la Khobar Towers, majengo ya makazi yaliyotumiwa kama makao ya wanajeshi wa Marekani. Mlipuko huo nusura uliharibu kabisa jengo lililokuwa karibu, ukawaua wanajeshi 19 wa Marekani na raia mmoja wa Saudia na kujeruhi mamia ya watu wengine kutoka mataifa mbalimbali.
Mnamo tarehe 21 mwezi Juni, mwaka 2001, jopo kuu la kusikiza kesi la mahakama ya serikali kuu ya Marekani liliwafungulia rasmi mashtaka watu 14 waliohusishwa na shambulio hilo. Miongoni mwa waliofunguliwa rasmi mashtaka walikuwa Ahmad Ibrahim al-Mughassil, Abdelkarim Hussein Mohamed al-Nasser, Ibrahim Salim Mohammed al-Yacoub, na Ali Saed bin Ali el-Hoorie, ambao kwa kila mmoja Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa.