Tovuti rasmi ya serikali ya Marekani

Shambulio la Bomu Dhidi ya Balozi za Marekani (Kenya na Tanzania)

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara

Tuzo

Up to $5 million

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu mashambulio ya mabomu ya mwaka 1998 dhidi ya Balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania. Mnamo tarehe 7 mwezi Agosti, mwaka 1998, wanachama wa kundi la kigaidi la al-Qa’ida (AQ) sawia walishambulia kwa mabomu Balozi za Marekani Nairobi na Dar es Salaam. Mashambulio hayo yaliwaua watu 224, yakawajeruhi wengine zaidi ya 5,000, na yakasababisha hasara kubwa kwenye majengo ya balozi hizo na uharibifu wa miundo iliyokuwa karibu.

Jijini Nairobi, magaidi walilipua lori lililobebeshwa vilipukaji karibu na maegesho ya ubalozi huo na kuwaua watu 213 — wakiwamo wafanyakazi 44 wa ubalozi (Wamarekani 12 na raia 32 wa mataifa ya kigeni) — na kuwajeruhi watu wengine 5,000, akiwamo Balozi wa Marekani Prudence Bushnell.

Jijini Dar es Salaam, magaidi walioendesha loriu lililobebeshwa vilipukaji walijaribu kuligonga lango la ubalozi, wakapiga risasi masijala ya ubalozi, na halafu wakalipua vilupukaji vyao. Mlipuko huo uliwaua watu 11 na kuwajeruhi 85.

Watu wafuatao walishtakiwa na kupatikana na hatia kwenye mahakama ya serikali kuu ya Marekani kuhusiana na mashambulio hayo:

  • Mamdouh Mahmud Salim, a founding member of AQ, was arrested in September 1998 in Germany and extradited to the United States. He is serving a life sentence in prison for his connection to the bombings.
  • In October 2001, AQ operatives Wadih El-Hage, Khalfan Khamis Mohamed, Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali, and Mohamed Sadeek Odeh were convicted on charges of planning and executing the bombings and sentenced to life in prison.
  • In January 2011, AQ operative Ahmed Khalfan Ghailani was convicted and sentenced to life for his role in the bombings.
  • In September 2014, Adel Abdel Bari, a close associate of AQ leader Ayman al-Zawahiri, pleaded guilty to conspiring to kill U.S. nationals and received a 25-year prison sentence. He was released from prison in 2020.
  • In May 2015, Khaled al-Fawwaz, deputy to now-deceased former AQ leader Usama bin Ladin, was sentenced to life in prison for his connection to the attacks.

Jopo la kusikiliza kesi la mahakama ya serikali kuu liliwafungulia rasmi mashtaka Abdullah Ahmed Abdullah, Anas al-Libi, Mohammed Atef, na Usama bin Ladin kwa majukumu yao katika mashambulio hayo. Wote wakiwa viongozi muhimu wa zamani wa AQ, sasa ni marehemu.

Tuzo kwa Mahakama pia tuzo zawadi kwa taarifa kuhusu kiongozi wa AQ Sayf al-Adl, ambaye alishtakiwa kwa jukumu lake katika milipuko ya Ubalozi.

Picha:

Mabango

Mahali Kunakohusiana:

Kenya, Tanzania

SUBMIT A TIP

Do Your Part. Secure a Safer World.

There are many ways to submit information to Rewards for Justice.

You may choose from multiple platforms and contact us in numerous languages. To process your information efficiently, we ask you to state your information as succinctly as possible, provide your name, location, and preferred language, and upload all relevant files such as photographs, videos, and documents to support your information. An RFJ representative will soon contact you. Please be patient, as RFJ reads every tip we receive.

Please open your Line app to submit a tip. The number is +1 202 702 7843

Please open your Viber app to submit a tip. The number is +1 202 702 7843

Please visit our Tor-based tips-reporting channel at: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Wasilisha Kidokezi

Fanya Jukumu Lako - Dhamini Ulimwengu Salama Zaidi

Zipo njia nyingi kuwasilisha kidokezo.

Unaweza kuchagua kutoka majukwaa mengi na kuwasiliana nasi katika lugha nyingi.
Kuchakata taarifa yako kwa ufanisi, tunakuomba kusema taarifa zako kwa maneno mafupi na Dhahiri iwezekanavyo, kutoa jina lako, mahali uliko, na lugha unayopendelea, na kupakia faili zote husika kama vile picha, video, na hati kuunga mkono taarifa yako. Mwakilishi wa TKM atawasliana nawe hivi karibuni. Tafadhali uwe na Subira, kwa kuwa TKM husoma kila kidokezo tunachopokea.

Tafadhali fungua programu yako ya Line ili kuwasilisha kidokezo. Nambari hiyo ni +1 202 718 4649

Tafadhali fungua programu yako ya Viber ili kuwasilisha kidokezo. Nambari hiyo ni +1 202 718 4649

Tafadhali tembelea idhaa yetu ya kuripotia vidokezo inayotumia mfumo wa TOR katika: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Skip to content