Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Seher Demir Sen, anayejulikana pia kama Munever Koz or Alba, kiongozi muhimu katika Chama/Umoja wa Kimapinduzi wa Ukombozi wa Watu (DHKP/C), iliyotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni. Shirika la DHKP/C limefanya mashambulio dhidi ya maslahi ya Marekani nchini Uturuki.
Sen alijiunga na shirika la Devrimci Sol (Dev Sol) mnamo mwaka 1980 na akabakia mwanachama hadi mwaka 1994 alipojiunga na DHKP/C baada ya Dev Sol kugawanyika. Alipanda ngazi hadi kufikia nafasi ya juu ya uongozi katika DHKP/C nchini Ugiriki, akiripotiwa kutumika kama mkuu wa ofisi ya kundi hilo jijini Athens. Sen ni mwanachama wa Kamati Kuu ya DHKP/C, iliyo chombo cha juu zaidi cha maamuzi cha kundi hilo.