Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kumi kwa taarifa itakayosababisha kuvurugwa kwa taratibu za kifedha za Hizballah.
Nazem Said Ahmad ni mtakatishaji pesa mashuhuri kutoka Lebanoni na mfadhili muhimu wa Hizballah.
Ahmad ni mmoja wa wafadhili wakuu wa Hizballah, akizalisha fedha kupitia mahusiano yake ya muda mrefu na biashara ya “almasi ya diamond”. Hizballah hutumia Ahmad na kampuni zake kutakatisha viwango vikubwa vya fedha zinakusudiwa kwenda kwa kundi hilo la kigaidi. Kufikia mwishoni mwa 2016, Ahmad alizingatiwa kama mfadhili mkuu ambaye aliitakatishia pesa Hizballah kupitia kampuni zake na binafsi alitoa fedha kwa Katibu Mkuu wa Hizballah, Hasan Nasrallah. Ahmad pia alihusika na magendo ya “almasi ya damu” na hapo awali aliendesha biashara nchini Ubelgiji ambazo ziliifaidi Hizballah.
Ahmad Ahmad huhifadhi baadhi ya fedha zake binafsi katika sanaa ya thamani ya juu katika jaribio la mapema la kupunguza athari za vikwazo vya Marekani, na alifungua jumba la sanaa Beirut kuonekana kama shughuli halali ili kutakatisha pesa. Ahmad ana mkusanyiko mkubwa wa sanaa yenye thamani ya mamilioni ya dola, zikiwemo kazi za Pablo Picasso na Andy Warhol, ambazo nyingi zimekuwa zikionyeshwa kwenye jumba lake la sanaa na fleti yake ghorofa ya juu huko Beirut. Kupitia uhamishaji wa fedha nyingi na miamala haramu ya fedha, Ahmad amejaribu kulinda mali zake kutozwa ushuru halali. Kwa kuficha kutoka kwa serikali ya Lebanoni faida haramu alizozipata, Ahmad ameinyima serikali na watu wa Lebanoni mapato ya ushuru yanayohitajika sana huku nchi hiyo ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi.
Mnamo tarehe 13, mwezi Desemba 2019, Wizara ya Hazina ya Marekani ilimtaja Ahmad kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224 kwa kusaidia kwa mali, kudhamini au kutoa usaidizi wa kifedha, mali au kiteknolojia, au wa bidhaa ama huduma kwa Hizballah au katika kuiunga mkono kundi hilo. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Ahmad katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Ahmad. Aidha, ni hatia kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa msaada wa nyenzo au raslimali kwa Hizballah, kundi lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni.