Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Muhammad Ahmed al-Munawar, anayejulikana pia kama Abdarahman al-Rashid Mansour na Ashraf Naeem Mansour. Al-Munawar, anayedaiwa kuwa mwanachama wa Shirika la kigaidi la Abu Nidal, anasakwa kwa jukumu lake katika utekaji nyara wa tarehe 5, mwezi Septemba, mwaka 1986 wa Ndege ya Pan Am 73 mjini Karachi, nchini Pakistani. Baada ya kuwashika mateka abiria 379 na wahudumu kwa karibu saa 16, watekaji nyara hao walianza kufyatua risasi kiholela. Watu ishirini, wakiwamo Wamarekani wawili, waliuliwa na wengine zaidi ya 100 wakajeruhiwa.
Kwa jukumu lake katika utekaji nyara huo, Al-Munawar alifunguliwa rasmi mashtaka na jopo kuu la kusikiliza kesi la mahakama ya serikali kuu ya Marekani na yupo kwenye Orodha ya Magaidi Wanaosakwa Zaidi ya Shirika la FBI. Al-Munawar inaelekea anaishi Mashariki ya Kati.