Tovuti rasmi ya serikali ya Marekani

Mtandao wa Haqqani (HQN)

Asia Kusini na Kati

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Mtandao wa Haqqani (HQN) ni shirika la wapiganaji linaloendesha shughuli zake nchini Afuganistani na Pakistani lililoundwa mwishoni mwa miaka ya elfu moja mia tisa na themanini. HQN limepanga na kutekeleza mashambulizi mengi makubwa na utekaji nyara dhidi ya wanajeshi wa Marekani na Majeshi ya Muungano nchini Afuganistani, serikali ya Afuganistani na shabaha za kiraia. Mnamo mwezi Juni, mwaka 2012, mshambuliaji wa kujitoa mhanga wa HQN alitekeleza shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani Khost, Afuganistani, akawaua wanajeshi wawili wa Marekani na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100. Maafisa wa serikali ya Afuganistani waliilaumu HQN kwa mlipuko wa bomu la kutegwa kwenye lori uliotokea mwezi Mei, mwaka 2017 mjini Kabul ambao uliwaua watu zaidi ya 150. HQN iliaminika kuhusika na shambulio la bomu la mwezi Januari, mwaka 2018, lililotegwa kwenye gari la kubebea wagonjwa mjini Kabul ambalo liliwaua watu zaidi ya 100. Maafisa wa Afghan pia waliilaumu HQN kwa shambulio la mwezi Januari, mwaka 2018, kwenye Hoteli ya Intercontinental mjini Kabul ambalo liliwaua watu 22.

Mnamo tarehe 19 mwezi Septemba, mwaka 2012, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja HQN kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Hapo awali, mnamo tarehe 7 mwezi Septemba, mwaka 2012, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani iliitaja HQN kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya HQN katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na HQN. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa HQN.

SUBMIT A TIP

Do Your Part. Secure a Safer World.

There are many ways to submit information to Rewards for Justice.

You may choose from multiple platforms and contact us in numerous languages. To process your information efficiently, we ask you to state your information as succinctly as possible, provide your name, location, and preferred language, and upload all relevant files such as photographs, videos, and documents to support your information. An RFJ representative will soon contact you. Please be patient, as RFJ reads every tip we receive.

Please visit our Tor-based tips-reporting channel at: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Wasilisha Kidokezi

Fanya Jukumu Lako - Dhamini Ulimwengu Salama Zaidi

Zipo njia nyingi kuwasilisha kidokezo.

Unaweza kuchagua kutoka majukwaa mengi na kuwasiliana nasi katika lugha nyingi.
Kuchakata taarifa yako kwa ufanisi, tunakuomba kusema taarifa zako kwa maneno mafupi na Dhahiri iwezekanavyo, kutoa jina lako, mahali uliko, na lugha unayopendelea, na kupakia faili zote husika kama vile picha, video, na hati kuunga mkono taarifa yako. Mwakilishi wa TKM atawasliana nawe hivi karibuni. Tafadhali uwe na Subira, kwa kuwa TKM husoma kila kidokezo tunachopokea.

Tafadhali tembelea idhaa yetu ya kuripotia vidokezo inayotumia mfumo wa TOR katika: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Skip to content