Tuzo kwa Mahakama inaahidi tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa zitakazowezesha kuvuruga taratibu za kifedha ya kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu la Iraki na Siria (ISIS). ISIS inategemea ufadhili na kuwezesha mitandao kuendeleza operesheni na kuanzisha mashambulizi nchini Syria na eneo zinazojirani.
Mitandao ya ISIS imefanya uhamisho wa fedha ili kusaidia juhudi za ISIS nchini Syria katika kambi za watu waliokimbia makaazi yao kwa kukusanya fedha nchini Indonesia na Uturuki, baadhi ambazo zilitumika kulipa wanaosafirisha watoto nje ya kambi na kuwapeleka kwa wapiganaji wa kigeni wa ISIS kama wanaoweza kuajiriwa.
Wanaohurumia ISIS katika zaidi ya nchi 40 wametuma pesa kwa watu wanaohusishwa na ISIS katika kambi hizi ili kuunga mkono ufufuo tena wa ISIS siku zijazo.Katika al-Hawi – ikiwa na takriban watu 70,000, kambi kubwa zaidi ya wakimbizi hao kaskazini-mashariki nchini ya Syria –wafuasi wa ISIS wamepokea hadi dola 20,000 kwa mwezi kupitia hawala, utaratibu wa uhamisho usio wa rasmi;nyingi ya uhamisho huo wa kifedha, umetoka nje ya nchi ya Syria au kupitia nchi jirani kama vile Uturuki.
Shughuli haramu za kuuza mafuta, ulanguzi wa vitu vya kale vilivyoporwa kutoka Siria na Iraki pia ni vyanzo muhimu ambavyo huleta pesa taslimu na kuwezesha ISIS kutekeleza mbinu zake za kinyama na kuwadhulumu raia wasio na hatia. Uharibifu na uporaji wa maeneo ya kihistoria unaofanywa na ISIS nchini Siria na Iraki umeharibu ushahidi usioweza kubadilishwa wa maisha ya kale na jamii.
Sarafu za kale na za kihistoria, vito vya thamani, mawe ya thamani yaliyochongwa, sanamu, medali za ukumbusho, na mawe yenye maadishi ya kale ni miongoni mwa vitu vya kitamaduni ambavyo ISIS imelangua. Kwa msaada kutoka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani, Baraza la Kimataifa la Majumba ya Makumbusho lilianzisha Orodha Nyekundu za Dharura za Vitu vya Kitamaduni vilivyo Hatarini ili kuwasilisha aina za vitu vya kitamaduni vilivyoporwa na kulanguliwa kutoka Siria na Iraki. Zinaweza kutazamwa hapa na hapa.