Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kumi kwa taarifa zitakazowezesha kuvurugwa kwa taratibu za kifedha za Hizballah. Mohammad Ibrahim Bazzi, ambaye huendesha shughuli au hufanya miamala ndani ya, au kupitia, Ubelgiji, Lebanoni, Iraki, na mataifa kadha Afrika Magharibi, ni mfadhili muhimu wa Hizballah. Bazzi ametengenezea Hizballah mamilioni ya dola kutoka kwa shughuli zake za kibiashara.
Bazzi ama anamiliki au anadhibiti kampuni za Global Trading Group NV, Euro African Group LTD, Africa Middle East Investment Holding SAL, Premier Investment Group SAL Offshore, na Car Escort Services S.A.L. Off Shore, zote zikiwa kampuni zilizowekewa vikwazo na Marekani na ambazo kupitia kwazo Bazzi ametoa mamilioni ya dola kwa Hizballah.
Mnamo tarehe 17 mwezi Mei, mwaka 2018, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja Mohammad Ibrahim Bazzi kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Bazzi katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Bazzi. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa Hizballah, kundi lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni.