Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Mohamed Makawi Ibrahim Mohamed. Alikuwa kiongozi wa shambulio lililowaua wafanyakazi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) John Granville na Abdelrahman Abbas Rahama mjini Khartoum mnamo tarehe mosi, mwezi Januari, mwaka 2008. Makawi alikuwa na ushirika na kundi la nchini Sudani liitwalo al-Qa’ida katika Ardhi ya Nile Mbili, ambalo lilikuwa limepanga kushambulia maslahi ya Marekani, Ulaya Magharibi, na Sudani.
Mahakama moja ya Sudani ilisikiliza kesi yake, ikampata na hatia na kumhukumu kifo Makawi mnamo mwaka 2009 kwa kuhusika kwake na mauaji hayo. Hata hivyo, Abdelbasit alitoroka gerezani mnamo tarehe 10 mwezi Juni, mwaka 2010, kabla ya hukumu yake kutekelezwa. Mpaka sasa angali mtoro na anaaminika kuwa yuko Somalia.
Mnamo tarehe 8 mwezi Januari, mwaka 2013, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Makawi kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Makawi katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Makawi.