Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Maalim Salman, kiongozi muhimu wa al-Shabaab, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni (FTO). Marehemu kiongozi wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane alimteua Salman kuwaongoza wapiganaji wa kigaidi wa kigeni Waafrika wa al-Shabaab. Akijulikana pia kama Maalim Salman Ali na Ameer Salman, Salman amehusika na shughuli zilizojikita Afrika zikilenga watalii, sehemu za burudani, na makanisa. Ingawa yeye huzingatia zaidi shughuli zilizo nje ya Somalia, Salman anajulikana kuishi Somalia, ambako huwafunza wapiganaji wa kigeni ili kutumwa kwingineko. Mnamo tarehe 24 mwezi Septemba, mwaka 2014, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Salman kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Salman katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Salman. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa FTO al-Shabaab.
Maalim Salman
Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara