Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni ishirini kwa taarifa zitakazowezesha kutambua aliko, kumwokoa na kumrejesha Robert A. “Bob”Levinson. Levinson, ambaye ni kachero maalumu wa Shirika la Upelelezi la FBI aliyestaafu, alitoweka akiwa katika safari ya kibiashara kwenye Kisiwa cha Kisha nchini Iran, mnamo tarehe 9, mwezi Machi, mwaka 2007. Levinson alikuwa amestaafu kutoka Shirika la Upelelezi la FBI mnamo mwaka 1998 na alikuwa akifanya kazi kama mchunguzi wa kibinafsi wakati wa kutoweka kwake.
Mnamo mwezi Disemba, mwaka 2020, Wizara ya Fedha ya Marekani iliwawekea vikwazo maofisa wawili wa ngazi za juu wa Iran, Mohammad Baseri na Ahmad Khazai, kwa kuhusika kwao katika utekaji nyara wa Levinson. Marekani inaendelea kutafuta taarifa kuwahusu wengine ambao walihusika.