Qa’ida nchini Iraq (AQI) Abu Bakr al-Baghdadi alimtuma kiongozi wa ANF Muhammad al-Jawlani nchini Syria kupanga vikundi vidogo vya kigaidi. Mnamo mwezi Aprili, mwaka 2013, al-Jawlani aliapa kutii kiongozi wa AQ Ayman al-Zawahiri. ANF ilijitenga kutoka AQI na kuwa kundi huru. Mnamo mwezi Januari, mwaka 2017, ANF iliungana na makundi mengine ya upinzani yenye siasa kali kuunda Hayat Tahrir al-Sham (HTS). ANF inasalia kuwa mshirika wa al-Qa’ida nchini Syria.
Lengo la ANF ni kuuondoa utawala wa rais wa Syria, Assad, na badala yake kuweka taifa la Kiislamu la dhehebu la Sunni. ANF ipo kwa wingi na inadhibiti sehemu ya eneo kaskazini magharibi mwa Syria, ambapo inaendeleza shughuli zake kama kundi la upinzani, na lina ushawishi wa viwango tofauti juu ya utawala wa ndani na njama za nje. ANF imetekeleza mashambulio kadha ya kigaidi kote nchini Syria, mara nyingi ikilenga raia.
Mnamo tarehe 15, mwezi Mei, mwaka 2014, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja ANF kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Awali, mnamo tarehe 14 mwezi Mei mwaka 2014, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje iliitaja ANF kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni Lenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Kutokana na kutajwa huku, mali yote na maslahi ya ANF katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na ANF. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama kutoa ufadhili wa nyenzo au rasilimali kwa ANF.