Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Ibrahim Ousmane, anayejulikana pia kama Dandou Cheffou, kwa kushiriki kwake katika shambulio la mwaka 2017 la Tongo Tongo, nchini Nijeri. Ibrahim Ousmane ni kamanda wa ISIS-Sahara Kuu (ISIS-GS).
Mnamo tarehe 4 mwezi Oktoba, mwaka 2017, karibu na kijiji cha Tongo Tongo, nchini Nijeri, wapiganaji wenye uhusiano na ISIS-GS waliwashambulia wanachama wa kikundi cha Vikosi Maalumu vya Marekani kilichopewa kazi ya kufunza, kushauri, na kusaidia vikosi vya Nijeri katika kukabiliana na ugaidi waliokuwa na jukumu la kufunza, kushauri, na kusaidia vikosi vya Nijeri kupambana na ugaidi. Shambulio hilo lilisababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Marekani na wanne wa Nijeri. Wamarekani wawili zaidi na Wanijeri wanane walijeruhiwa katika tukio hilo. Mnamo tarehe 12 mwezi Januari, mwaka, 2018, kiongozi wa ISIS-GS Adnan Abu Walid al-Sahrawi alidai kuhusika na shambulio hilo.