Hurras al-Din (HAD) ni kundi la wapiganaji wa Kiislamu mshirika wa al-Qa’ida lililoibuka nchini Syria mapema mwaka 2018 baada ya vikundi kadha kujitenga kutoka Hayat Tahrir al-Sham (HTS).
Mnamo tarehe 10 mwezi Septemba, mwaka 2019, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja HAD kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya HAD katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na HAD.