Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni mbili kwa taarifa kumhusu Hafiz Abdul Rahman Makki, anayejulikana pia kama Abdulrahman Maki. Makki ameshikilia majukumu mbalimbali ya uongozi katika Lashkar-e-Tayyiba (LeT), kundi lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni (FTO). Pia ameshiriki katika kuchangisha pesa kwa ajili ya shughuli za LeT.
Mnamo mwaka 2020, mahakama ya kupambana na ugaidi ya Pakistani ilimpata Makki na hatia kwa kosa moja la kufadhili ugaidi na ikamhukumu kifungo cha gerezani. Marekani inaendelea kutafuta taarifa kumhusu Makki kwa sababu mfumo wa mahakama wa Pakistani umewaachilia huru viongozi na majasusi wa LeT waliopatwa na hatia hapo awali.
Mnamo tarehe 4 mwezi Novemba, mwaka 2010, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja Makki kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Makki katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Makki. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa FTO LeT.