Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Faruq al-Suri, anayejulikana pia kama Samir Hijazi au Abu Hammam al-Shami. Al-Suri ndiye kiongozi wa kundi la kigaidi la Hurras al-Din (HAD) na mwanachama mkonge wa al-Qa’ida (AQ).
Al-Suri alikuwa mkufunzi mwandamizi wa kijeshi pamoja na kiongozi mwandamizi wa AQ Sayf al-Adl nchini Afuganistani miaka ya tisini, na pia aliwafunza wapiganaji wa AQ nchini Iraki kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2005. Awali Al-Suri alizuiliwa nchini Lebanoni kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2013 na baadaye akawa kamanda wa kijeshi wa Vuguvugu la al-Nusrah (ANF). Aliondoka ANF mnamo mwaka 2016.
Mnamo tarehe 10 mwezi Septemba, mwaka 2019, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja al-Suri kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya al-Suri katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na al-Suri.