Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Aziz Haqqani, anayejulikana pia kama Abdul Aziz Haqqani. Aziz ni kiongozi muhimu wa mfumo Mtandao wa Haqqani (HQN), kundi lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni (FTO), na ndugu wa kiongozi wa HQN na naibu kiongozi wa Taliban Sirajuddin Haqqani.
Aziz amehusika na kupanga na kutekeleza mashambulio ya vilipukaji vya kujitengenezea dhidi ya shabaha za serikali ya Afuganistani, na aliwajibikia mashambulio yote makubwa ya HQN baada ya kifo cha kaka yake, Badruddin Haqqani. Aziz amehusika kindani katika shughuli za ugavi na usafirishaji wa vifaa na maamuzi ya kivita katika mashambulio ya HQN dhidi ya majeshi ya Afuganistani na ya Muungano kwenye mpaka wa Afuganistani na Pakistani. Zaidi, ametumika kama kiunganishi cha kimsingi cha HQN kwa shughuli mjini Kabul na mashambulio ya hali ya juu kote nchini Afuganistani.
Mnamo tarehe 25 mwezi Agosti, mwaka 2015, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Aziz Haqqani kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Aziz Haqqani katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Aziz Haqqani. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa FTO HQN.