Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kumi kwa taarifa zitakazowezesha kuvurugwa kwa taratibu za kifedha za Hizballah. Ali Youssef Charara, anayejulikana pia kama Ali Youssef Sharara na ‘Ali Yusuf Sharara, ni mfadhili muhimu wa Hizballah na Mwenyekiti na Meneja Mkuu kampuni ya mawasiliano ya simu yenye makao yake nchini Lebanoni, Spectrum Investment Group Holding SAL, taasisi iliyowekewa vikwazo na Wizara ya Fdha ya Marekani. Charara amepokea mamilioni ya dola kutoka kwa Hizballah ili kuwekeza kwenye miradi ya kibiashara ambayo huunga mkono kifedha kundi hilo la kigaidi.
Zaidi ya Charara kuwezesha uwekezaji wa kibiashara, kwa niaba ya Hizballah, pia amefanya kazi katika ujasiriamali wa mafuta nchini Iraki. Aidha, Charara ana biashara nyingi kwenye tasnia ya mawasiliano ya simu Afrika Magharibi.
Mnamo tarehe 7 mwezi Januari, mwaka 2016, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja Charara kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Charara katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Charara. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa Hizballah, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni.