Tovuti rasmi ya serikali ya Marekani

Ali Sayyid Muhamed Mustafa al-Bakri

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kwa taarifa kumhusu Ali Sayyid Muhamed Mustafa al-Bakri, anayejulikana pia kama Abd al-Aziz al-Masri. Al-Bakri ni mwanachama wa baraza la shura la al-Qai’da (AQ), jopo la maamuzi la kundi hilo, na ni mshirika wa karibu wa viongozi wa AQ Sayf al-Adl na Ayman al-Zawahiri. Al-Bakri ni bingwa wa vilipuzi na silaha za kemikali.

Kabla ya kujiunga na AQ, al-Bakri alikuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Jihad ya Kiislamu la Misri chini ya uelekezi wa al-Zawahiri. Alitumika kama mkufunzi kwenye kambi za AQ nchini Afuganistani, akifunza magaidi kurutu jinsi ya kutumia vilipuzi na silaha za kemikali. Al-Bakri pia alijaribu kuteka nyara ndege ya abiria ya kampuni ya Pakistani Air mnamo Disemba 2000. Inawezekana kwamba anaendelea kuwafunza magaidi wa AQ na watu wengine wenye itikadi kali.

Al-Bakri anaishi na familia yake nchini Irani.

Mnamo tarehe 3 mwezi Oktoba, mwaka 2005, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja al-Bakri kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya al-Bakri katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na al-Bakri. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa AQ, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni.

Picha:

Mabango

Mahali Kunakohusiana:

Iran

Tarehe ya Kuzaliwa:

Mnamo tarehe 18, mwezi Aprili, mwaka 1966

Mahali pa Kuzaliwa:

Bani Suwayf, Misri

Utaifa:

Misri

Jinsia:

Mwanamume

Rangi ya Macho:

Nyeusi

Lakabu/Tahajia Mbadala za Majina:

Ali Sa’d Muhammad Mustafa Bakri; Abd al-Aziz al-Masri; Hasan ‘Umar Ibrahim Ali Saleem Abu Salsbil; Abu Salsabil Hassan Omar; Hasan ‘Umar Zizo

SUBMIT A TIP

Do Your Part. Secure a Safer World.

There are many ways to submit information to Rewards for Justice.

You may choose from multiple platforms and contact us in numerous languages. To process your information efficiently, we ask you to state your information as succinctly as possible, provide your name, location, and preferred language, and upload all relevant files such as photographs, videos, and documents to support your information. An RFJ representative will soon contact you. Please be patient, as RFJ reads every tip we receive.

Wasilisha Kidokezi

Fanya Jukumu Lako - Dhamini Ulimwengu Salama Zaidi

Zipo njia nyingi kuwasilisha kidokezo.

Unaweza kuchagua kutoka majukwaa mengi na kuwasiliana nasi katika lugha nyingi.
Kuchakata taarifa yako kwa ufanisi, tunakuomba kusema taarifa zako kwa maneno mafupi na Dhahiri iwezekanavyo, kutoa jina lako, mahali uliko, na lugha unayopendelea, na kupakia faili zote husika kama vile picha, video, na hati kuunga mkono taarifa yako. Mwakilishi wa TKM atawasliana nawe hivi karibuni. Tafadhali uwe na Subira, kwa kuwa TKM husoma kila kidokezo tunachopokea.

Skip to content