Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kumi kwa taarifa zitakazosaidia kuvuruga taratibu za kifedha za Hizballah. Ali Qasir ni mwakilishi wa Hizballah nchini Irani na ni mwezeshaji muhimu wa shughuli za kifedha na kibiashara ambazo hunufaisha kikosi cha Irani cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu-Kikosi cha Qods (IRGC-QF) na Hizballah. Yeye pia ni mpwa wa ofisa wa Hizballah, Muhammad Qasir, ambaye huwa anafanya kazi naye kwa karibu ili kufanikisha shughuli za kifedha kati ya IRGC-QF na Hizballah.
Ali Qasir pia ndiye mkurugenzi msimamizi wa kampuni iliyo na uhusiano na Hizballah na inayoendesha shughuli zake wazi badala ya Hizballah, Talaqi Group, ambayo hufadhili usafirishaji wa mafuta kwa IRGC-QF. Ali Qasir huvipa kazi vyombo vya majini ya kupelekea mtandao huo wa kigaidi mafuta kuambatana na ushauri wa IRGC-QF. Majukumu ya Ali Qasir ni pamoja na kufanya mashauri kuhusu bei ya mauzo ya bidhaa na kupanga malipo yanayohusiana na vyombo vya uchukuzi. Ali Qasir amesimamia mashauri ya bei ya mauzo na akatoa ushirikiano kugharamia na kuwezesha usafirishaji wa mafuta ya Iran na ADRIAN DARYA 1 kwa manufaa ya IRGC-QF. Ali Qasir huwakilisha kampuni ya Hokoul S.A.L. Offshore iliyo na makao yake nchini Lebanon katika mashauri kuhusu kuiuzia Syria mafuta yasiyochakatwa ya Iran. Vilevile, Ali Qasir amepanga na kufanya kazi na wengine kutumia Talaqi Group ili kufanikisha uuzaji wa vyuma vya thamani ya makumi ya mamilioni ya dola.
Mnamo tarehe 4, mwezi Septemba, mwaka 2019, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja Ali Qasir kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Kutokana na kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, mali yote na maslahi ya Ali Qasir katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Ali Qasir. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa Hizballah, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni.