Al-Qa’ida Kwenye Rasi ya Kiarabu (AQAP) ni kundi lenye itikadi kali lenye makao yake nchini Yemeni na ambalo liliibuka mnamo mwezi Januari, mwaka 2009 baada ya muungano wa makundi ya kigaidi ya Yemeni na Saudia. Malengo ya AQAP ni pamoja na kuanzisha milki ya khalifa na kutekeleza sharia kwenye Rasi ya Kiarabu na maeneo ya Mashariki ya Kati. AQAP imelenga maslahi ya ndani, ya Marekani, na Magharibi yaliyoko Rasi ya Kiarabu, pamoja na ng’ambo. Kundi hili limedai kuwajibika na vitendo vingi vya kigaidi, ikiwa ni pamoja na shambulio la mwezi Januari, mwaka 2015 dhidi ya ofisi za gazeti la kidhihaka, Charlie Hebdo, jijini Paris, ambalo liliua watu 12.
AQAP ni mshirika wa AQ na kadhi mkuu wa AQAP hushirikiana kwa karibu na viongozi wa AQ kupanga mashambulio. Mlipuaji bomu wa AQAP, al-Asiri, aliunda bomu la chupi lililokusudiwa kutumika katika njama ya kulipua ndege siku ya Krismasi mnamo mwaka 2012 na pia alituma mabomu kwenda Marekani yaliyofichwa ndani ya mashine za kupiga chapa kwa kutumia matarishi.
Mnamo tarehe 19, mwezi Januari, mwaka 2010, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja AQAP kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa, na kama Gaidi wa kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ni kwamba, mali yote na maslahi ya AQAP katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na AQAP. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa AQAP.