Al-Qa‘ida (AQ) ilipangwa na Usama bin Ladin mnamo mwaka 1988 ikiwa na Waarabu waliopigana nchini Afuganistani dhidi ya vikosi vya kijeshi vilviyoikalia nchi hiyo vya Muungano wa Kisovieti uliovunjika sasa. AQ hujitahidi kuondoa ushawishi wa Ulaya Magharibi kutoka mataifa ya Kiislamu, kupindua serikali za ‘uasi’ za mataifa ya Kiislamu, na kuanzisha ukhalifa wa Kiislamu unaotawaliwa kwa ufasiri wa AQ wa sharia na ambayo hatimaye itakuwa kitovu katika mpangilio mpya wa kimataifa. Kimsingi malengo haya hayajabadilishwa tangu kundi hilo litangaze vita hadharani dhidi ya Marekani. AQ imepoteza majasusi wengi wa viwango vya kadiri na vya juu kutotana na juhudi za kukabiliana na ugaidi, lakini inaendelea kusajili, kupanga, kuhimiza, na kutekeleza mashambulio. AQ ina mashirika inayoshirikiana nayo katika maeneo ya Mashariki ya Kati, Afrika, na Asia na nguvu zake kwa sasa kimsingi zipo kwenye makundi-shirika hayo.
AQ imehusika na mashambulio mengi makubwa na yenye majeruhi wengi. AQ ilitekeleza mashambulio matatu ya mabomu dhidi ya wanajeshi wa Marekani kwenye eneo la Aden, nchini Yemen mnamo mwaka 1992 na ikadai kuangusha kwa makombora helikopta za Marekani na kuwaua wanajeshi wa Marekani nchini Somalia mnamo mwaka 1993. AQ pia ilitekeleza mashambulio ya mabomu mnamo mwaka 1998 dhidi ya Balozi za Marekani mijini Nairobi na Dar es Salaam yaliyowaua watu 224 na kuwarejuhi wengine zaidi ya 5,000. Mnamo mwezi Oktoba mwaka 2000, AQ ilitekeleza shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya meli ya USS Cole kwenye bandari ya Aden kwa kutumia boti iliyojazwa vilipuzi, shambulio ambalo liliua mabaharia 17 wa Jeshi la Majini la Marekani na kujeruhi zaidi ya 30. Mnamo mwezi Septemba 11 mwaka 2001, wanachama 19 wa AQ waliteka na kuangusha ndege nne za abiria za Kimarekani – mbili kwenye jumba la World Trade Center jijini New York, moja Pentagon, na ya mwisho kwenye shamba lililo katika eneo la Shanksville, Pennsylvania. Mashambulio hayo ya 9/11 yaliua karibu watu 3,000.
Mnamo tarehe 8 mwezi Oktoba, mwaka 1999, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marerkani ilitaja AQ kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Mnamo tarehe 23 mwezi Septemba, mwaka 2001, AQ iliorodheshwa kwenye Kiambatanisho cha Amri ya Rais 13224. Kutokana na kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, mali yote na maslahi ya AQ katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na AQ. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa msaada wa nyenzo au rasilimali kwa AQ.