Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni 10 kwa taarifa kumhusu Ahmed Diriye, anayejulikana pia kama Ahmed Umar na Abu Ubaidah. Abu Ubaidah anahudumu kama kiongozi wa al-Shabaab — nafasi ambayo ameishikilia tangu kifo cha kiongozi wa zamani wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane. Abu Ubaidah alikuwa mmoja wa wandani wa Godane wakati wa kifo cha Godane.
Kabla ya kuchukua nafasi ya Godane, Abu Ubaidah alitumika katika nyadhifa tofauti ndani ya al-Shabaab, zikiwamo kama msaidizi wa Godane, naibu gavana wa eneo la Lower Juba la Somalia mnamo mwaka 2008, na gavana wa al-Shabaab maeneo ya Bay na Bakool ya Somalia mnamo mwaka 2009. Kufikia mwaka 2013, alikuwa mshauri mwandamizi wa Godane, na alitumika katika “Idara ya Ndani” ya al-Shabaab, ambapo alisimamia shughuli za ndani za kundi hilo. Anashiriki maono ya Godane kwa mashambulio ya kigaidi ya al-Shabaab nchini Somalia kama kipengele cha matamanio makubwa ya kimataifa ya al-Qa’ida.
Mnamo tarehe 21 mwezi Aprili, mwaka 2015, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Ubaidah kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Ubaidah katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Ubaidah. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa al-Shabaab, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni.