Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Abdul Wali, anayejulikana pia kama Omar Khalid Khorasani. Wali ndiye kiongozi wa Jamaat ul-Ahrar (JuA), mrengo wa kivita unaoshirikiana na Tehrik-e Taliban Pakistan (TTP), kundi lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni. Chini ya uongozi wa Wali, JuA limekuwa mojawapo ya makundi ya mitandao ya TTP yenye harakati nyingi zaidi kwenye Mkoa wa Punjab, nchini Pakistan na limedai kuhusika na mashambulio mengi kote Pakistani.
Wali anaripotiwa kuendesha shughuli zake kwenye mikoani Nangarhar na Kunar nchini Afuganistani. Wali alizaliwa katika Mohmand Agency, Pakistan. Yeye ni mwanahabari wa zamani na mshairi na alisoma kwenye shule kadha za madrasa mjini Karachi, Pakistani.