Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Abdikadir Mohamed Abdikadir, anayejulikana pia kama Ikrima. Abdikadir ni kiongozi wa ngazi ya juu wa al-Shabaab na ametumika kama Mkuu wa Shughuli na Mipangilio. Abdikadir pia ameelekeza mipango ya awali ya mashambulio ya al-Shabaab. Ameratibu usajili wa vijana wa Kenya kujiunga na al-Shabaab na akawa kamanda wa kikosi cha wapiganaji Wakenya wa al-Shabaab nchini Somalia.
Mnamo tarehe 6 mwezi Agosti, mwaka 2021, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Abdikadir kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Abdikadir katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Abdikadir. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa al-Shabaab, kundi lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni.