Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Abdelbasit Alhaj Alhassan Haj Hamad. Abdelbasit anasakwa kutokana na jukumu lake kama mmoja wa watu wenye bunduki kwenye mauaji ya John Granville na Abdelrahman Abbas Rahama, wafanyakazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) jijini Khartoum mnamo tarehe mosi Januari, mwaka 2008.(USAID) kule Khartoum mnamo tarehe 1 Januari, 2008.
Mahakama ya Sudani ilisikiliza kesi yake Abdelbasit, ikampata na hatia na kumhukumu kifo mnamo mwaka 2009 kwa kuhusika kwake na mauaji hayo. Hata hivyo, Abdelbasit alitoroka gerezani mnamo tarehe 10 mwezi Juni, mwaka 2010, kabla hukumu yake haijatekelezwa. Mpaka sasa angali mtoro na anaaminika kuwa yuko Somalia.
Mnamo tarehe 8 mwezi Januari mwaka 2013, Abdelbasit alitajwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, mali yote na maslahi ya Abdelbasit katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Abdelbasit.