Tovuti rasmi ya serikali ya Marekani

Kuhusu

Muhtasari wa Programu

Historia ya Programu na Mamlaka za Kisheria

TKM, programu ya tuzo kwa usalama wa kitaifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ilianzishwa mwaka 1984 na Sheria ya Kukabiliana na Ugaidi wa Kimataifa, Sheria ya Umma 98-533 (iliyopangwa wazi katika 22 U.S.C. § 2708). Chini ya usimamizi wa Ofisi ya Usalama wa Kidiplomasia ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, dhamira ya TKM ni kutoa tuzo ili kupata taarifa inayolinda maisha ya Wamarekani na maslahi ya Marekani na kuendeleza usalama wa kitaifa wa Marekani.

Tangu mwaka 1984, Bunge limepanua mamlaka ya kisheria ya TKM kutoa tuzo kwa habari katika nyanja tatu pana:

 • Ugaidi. Kwa taarifa ambayo:
  • Inapelekea kukamatwa au kutiliwa hatiani kwa yeyote anayepanga, kutenda, kusaidia, au kujaribu vitendo vya kigaidia vya kimataifa dhidi ya Wamarekani au mali ya Marekani ndani ya Marekani au ng’ambo;
  • Inazuia kitendo kama hicho kwanza kisitokee;
  • Inamtambulisha au kutambulisha mahali alipo kiongozi muhimu wa kigaidi; au
  • Inavuruga mifumo ya kifedha ya makundi ya kigaidi ya kigeni. Hii ni pamoja na kuvuruga mifumo mitandao ya utekaji nyara na matukio ya utekaji nyara ambayo yanaunga mkono kifedha mashirika kama hayo.
 • Shughuli Mtandaoni Zenye Nia Mbaya. Kwa taarifa ambayo:
  • Inamtambulisha au kutambulisha mahali alipo mtu yeyote ambaye, kwa maelekezo au chini ya udhibiti wa serikali ya kigeni, anasaidia au kushiriki katika ukiukaji wa Sheria ya Ulaghai na Matumizi Mabaya ya Kompyuta (“CFAA”), 18 U.S.C. § 1030. Hii ni pamoja na kuingilia uchaguzi wa nchi nyingine.
 • Korea Kaskazini. Kwa taarifa ambayo:
  • Inavuruga mifumo ya kifedha ya watu au vyombo husika katika shughuli fulani za kuunga mkono utawala wa Korea Kaskazini, au
  • Inamtambulisha au kutambulisha mahali alipo mtu yeyote ambaye, kwa maelekezo au chini ya udhibiti wa serikali ya Korea Kaskazini anasaidia au kushiriki katika ukiukaji wa Sheria ya Ulaghai na Matumizi Mabaya ya Kompyuta (“CFAA”), 18 U.S.C. § 1030. Hii ni pamoja na mashambulio ya kimtandao na madukizo kwenye mifumo ya serikali ya Marekani.

Kutangaza Ahadi za Tuzo

Mara Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje ameidhinisha kutolewa kwa ahadi ya tuzo, TKM inaitangaza na kushirikiana na hadhira inayolengwa kwa njia inayofaa kitamaduni kwa kutumia vifaa mbalimbali, vikiwemo mitandao ya kijamii, programu za gumzo za kijamii, na vyombo vya habari vya jadi.

Kuchakata Vidokezo

Matangazo ya TKM huwaelekeza watu kutuma ujumbe wa taarifa zao kwa namba za simu za TKM za kupokea vidokezo katika lugha mahususi kupitia programu kadhaa za kutuma ujumbe zinazopatikana na zilizosimbwa, zikiwemo Selo, Telegramu, na WhatsApp. Watu binafsi pia wanaweza kuwasilisha taarifa zao kupitia kwa baruapepe na akaunti za mitandao ya kijamii.TKM husambaza taarifa ya vidokezo inayofaa kwa mashirika mengine ya serikali ya Marekani.

Malipo ya Tuzo

Iwapo taarifa iliyotolewa na kijumbe mtoa habari inaleta matokeo chanya, shirika la serikali ya Marekani linalohusika na uchunguzi wa kesi hiyo linaweza kuamua kumteua mtoa habari huyo kwa malipo ya tuzo. Uteuzi kwa malipo hupitiwa na kamati ya mashirika mbalimbali na halafu kutumwa kwa Waziri kuamua iwapo malipo yatatolewa.

Tangu mwanzo wa Tangu mwanzo wa programu ya Tuzo kwa Mahakama mnamo mwaka 1984, Serikali ya Marekani imelipa zaidi ya dola milioni $250 kwa zaidi ya watu 125 waliotoa taarifa zilizosababisha magaidi kufikishwa mahakamani, zilizovuruga mashambulio au ugharamiaji wa magaidi, au kuvuruga mifumo ya kifedha ya wale wanaoshiriki katika shughuli zisizo halali kuunga mkono utawala wa Korea Kaskazini.

SUBMIT A TIP

Do Your Part. Secure a Safer World.

There are many ways to submit information to Rewards for Justice.

You may choose from multiple platforms and contact us in numerous languages. To process your information efficiently, we ask you to state your information as succinctly as possible, provide your name, location, and preferred language, and upload all relevant files such as photographs, videos, and documents to support your information. An RFJ representative will soon contact you. Please be patient, as RFJ reads every tip we receive.

Wasilisha Kidokezi

Fanya Jukumu Lako - Dhamini Ulimwengu Salama Zaidi

Zipo njia nyingi kuwasilisha kidokezo.

Unaweza kuchagua kutoka majukwaa mengi na kuwasiliana nasi katika lugha nyingi.
Kuchakata taarifa yako kwa ufanisi, tunakuomba kusema taarifa zako kwa maneno mafupi na Dhahiri iwezekanavyo, kutoa jina lako, mahali uliko, na lugha unayopendelea, na kupakia faili zote husika kama vile picha, video, na hati kuunga mkono taarifa yako. Mwakilishi wa TKM atawasliana nawe hivi karibuni. Tafadhali uwe na Subira, kwa kuwa TKM husoma kila kidokezo tunachopokea.

Skip to content