Tovuti rasmi ya serikali ya Marekani

Kuhusu

Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara

TKM ni programu ya tuzo ya mashirika kwa pamoja iliyoanzishwa na Sheria ya Kupambana na Ugaida wa Kimataifa ya mwaka 1984, Sheria ya Umma 98-533 (iliyopangwa wazi katika 22 U.S.C. § 2708) na kusimamiwa na Ofisi ya Usalama wa Kidiplomasia ya Wizara ya Mambo ya Nje.

Dhamira ya TKM ni kutoa taarifa zinazosaidia kulinda usalama wa kitaifa wa Marekani.

Chini ya mamlaka ya kisheria ya mwaka 1984, dhamira asili ya TKM ilikuwa kutoa tuzo kwa taarifa ambayo

  • Inapelekea kukamatwa au kutiliwa hatiani mtu yeyote anayepanga, kutekeleza, kusaidia, au anajaribu matendo ya ugaidi wa kimataifa dhidi ya watu au mali ya Marekani
  • Inazuia kutokea hapo kwanza kwa matendo kama hayo
  • Inapelekea kutambuliwa au mahali aliko kiongozi mkuu wa kigaidi
  • Inavuruga ufadhili kifedha wa ugaidi

 

Mwaka 2017, Bunge lilirekebisha mamlaka ya kisheria ya TKM yawe ni pamoja na kutoa tuzo kwa habari inayopelekea

  • Kuvuruga mifumo ya kifedha ya watu wanaoshiriki kwa shughuli fulani za kuunga mkono utawala wa Korea Kaskazini
  • Kutambuliwa au mahali aliko yeyote ambaye kwa maelekezo au chini ya udhibiti wa serikali ya kigeni, anasaidia au kushiriki kwenye ukiukaji wa Sheria ya Udaganyifu na Matumizi mabaya ya Kompyuta (kuingilia kompyuta bila ruhusa na aina zingine za hila zinazohusu kompyuta)

 

Ahadi za tuzo zinaweza kuanzia chini ya dola milioni moja hadi dola milioni 25.

TKW inaweza kulipa tuzo kwenye matukio ambapo hakuna ahadi ya awali kutoa tuzo.

Tangu mwanzo wake, TKM imelipa zaidi ya dola milioni $250 kwa zaidi ya watu 125 waliotoa taarifa za maana zilizosaidia kulinda usalama wa kitaifa wa Marekani.

Juhudi hizi zimeokoa maisha yasiyohesabika.

Pamoja na tovuti ya TKM, tunatumia lugha za hadhira husika katika majukwaa ya mitandao ya kijamii, mabango, foda ndogo za njiti za kiberiti, matangazo ya kulipia ya radio na magazeti, mtandao na njia zingine zozote za kufaa kuwasiliana na watu ambao huenda wakawa na habari husika ya kutoa.

Usiri ni kipengele muhimu cha programu ya TKM. Hatufichui hadharani habari mahususi zilizowasilishwa kama jibu la ahadi yetu ya tuzo au majina ya watu wanaopokea malipo ya tuzo, na kwa kawaida hata hatufichui kwamba tuzo fulani limekwisha lipwa. Kwenye baadhi ya kesi umaarufu wa juu, huenda tukatangaza malipo ya tuzo, lakini sio taarifa zilizotolewa au jina la yule aliyeziwasilisha habari.

Mnamo mwezi Februari mwaka 1995, Ramzi Yousef, mmoja wa washambuliaji kwa bomu wa jumba la World Trade Center mwaka 1993 alipatikana na kukamatwa nchini Pakistani kutokana na habari za mtu chanzo cha habari aliyeitikia ahadi ya tuzo kutoka kwa TKM.

TKM pia imelipa tuzo nyingi kwa watu binafsi kwenye sherehe nne tofauti za hadhara za kutoa malipo nchini Filipino. Mnamo tarehe 7 Juni 2007, kwenye sherehe ya hadhara, TKM ililipa jumla ya dola milioni kumi. Haya ni malipo ya juu zaidi nchini Filipino tangu programu hii ilipoanza.

TKM ililipa tuzo ya dola milioni tatu kwa mtu aliyetoa taarifa zilizopelekea kukamatwa na kutiliwa hatiani kwa gaidi kiongozi Ahmed Abu Khattalah, mwanzilishi mwamba wa shambulio la mwaka 2012 dhidi ya jengo la muda na jingine dogo lililounganishwa ya ujumbe wa Marekani mjini Benghazi, Libya, lililowaua Wamarekani wanne, akiwemo balozi wa Marekani.

Kama ilivyotajwa, TKM mara kwa mara hutoa matangazo ya kiwango kidogo kuhusu malipo ya tuzo yenye umaarufu wa juu.

Tunatoa pia ripoti ya siri kwa Bunge baada ya malipo kutolewa.

Watu wanaweza kustahiki tuzo kama wakitoa taarifa ambazo:

  • Zinasaidia kuzuia au kwa njia ya kufaa zinatatua matendo ya ugaidi wa kimataifa dhidi ya mali au raia wa Marekani kokote duniani.
  • Zinawezesha kutambulika au kupatikana aliko kiongozi muhimu katika shirika la kigaidi la kigeni.
  • Inavuruga mifumo ya kifedha ya watu binafsi au vyombo vinavyoshiriki katika shughuli za kuunga mkono utawala wa Korea Kaskazini.
  • Zinawezesha kutambulika au kupatikana kwa mtu binafsi yeyote ambaye, kwa maelekezo au chini ya udhibiti wa serikali ya kigeni, anasaidia au kushiriki kwenye ukiukaji wa Sheria ya Udaganyifu na Matumizi Mabaya ya Kompyuta.

 

Maofisa wa serikali kwa jumla sio wastahilifu kupata tuzo isipokuwa wakitoa taarifa lakini nje ya utendaji wa wajibu wao rasmi.

Usiri ni jiwe la pembeni la programu ya TKM. TKM inaweka siri kali utambulisho wa watu wanaotoa taarifa kwa siri na wale wanaopokea malipo ya tuzo. Aidha, kuzingatia kesi kwa kesi, uhamisho unaweza kupatikana kwa mtu anayetoa taarifa kwa siri, yeye na familia yake.

Malipo ya tuzo ya TKM ni mchakato wa mashauriano:

  • Ofisi ya uchunguzi ya Marekani (kama vile Wizara ya Ulinzi au FBI) au ubalozi wa Marekani ng’ambo lazima kwanza kuteua mtu kupata tuzo. Watu wanaodai kutoa taarifa hawawezi kujiteua kwa malipo ya tuzo.
  • Baada ya ukaguzi rasmi kisheria wa ustahimilifu, kamati ya mashirika basi hutathmini kwa uangalifu taarifa zilizotolewa na ofisi teuzi. Baada ya mashauriano kuhusu ustahili wa uteuzi, kamati hutoa pendekezo kwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.
  • Pendekezo la kamati hata hivyo sio lazima lifuatwe. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje ana hiari kamili iwapo ataidhinisha au atakata tuzo yoyote, na anaweza kubadilisha kiasi cha tuzo, kulingana na masharti ya sheria.
  • Kabla ya kulipa tuzo kwenye jambo ambalo utawala wa shirikisho una mamlaka ya jinai juu yake, Mkuu wa Sheria lazima kuafikiana na Waziri.
  • Uteuzi sio hakikisho la kuidhinishwa kwa malipo. Uamuzi wa Waziri kutoa malipo ni wa mwisho na wa kuthibitika na usiotegemea kupitiliwa upya na mahakama.

Kiasi cha malipo ya tuzo hutegemea mambo kadhaa, ikiwemo lakini sio tu: thamani ya taarifa zilizotolewa; kiwango cha tishio kilichopunguzwa na taarifa zilizopokelewa; ukali wa hatari au majeraha kwa raia wa Marekani au mali ambayo ingesababishwa na tishio; hatari inayomkabili mtu anayetoa habari za siri na familia yake; na kiwango cha ushirikiano wa anayetoa taarifa kwa siri. Hakuna malipo yanayotolewa badala ya ushuhuda.

Malipo kwa mtu anayetoa habari kwa siri yanaweza kuwa kiasi chochote hadi kufikia jumla ya dola kama ilivyotangazwa kwenye ahadi ya tuzo.

Ndiyo, kwa miaka mingi Tuzo kwa Mahakama imewaondoa washukiwa mbalimbali kwenye orodha yake, akiwemo kiongozi wa kundi la al-Qa’ida Usama bin Ladin na kiongozi wa ISIS Abu Bakr al-Baghdadi.

Washukiwa wanaweza kuondolewa kwenye orodha ya TKM kwa sababu anuwai, ikiwa ni pamoja na wanapokamatwa na vyombo vya sheria au vikosi vya usalama, inapothibitishwa kuwa wamekufa, au vinginevyo kutangazwa na chanzo rasmi kutokuwa tishio tena.

Tunakatisha tamaa vikali wawindaji wa watoro na wengine wasio wa serikali kutofuatilia kukamatwa kwa magaidi au watu wengine wanaotafutwa; badala yake, TKM hutoa tuzo kwa taarifa zitakazowezesha mamlaka zinazofaa za serikali kutafuta na kuwakamata watu kama hao.

Watu walio na taarifa wanafaa kuituma kwa njia ya ujumbe mfupi kwa TKM kupitia mitandao ya WhatsApp, Telegramu, au Selo nambari (202) 702-7843.

Watu binafsi wanaweza pia kuwasilisha taarifa kwa kuwasiliana na Afisa Usalama wa Mkoa katika ubalozi au ubalozi mdogo ulio karibu, au ofisi ya shirika la FBI iliyo karibu.

Isipokuwa haki ya kunakili imeashiriwa, taarifa katika tovuti hii zinapatikana kwa umma na zinaweza kutolewa tena, kuchapishwa au vinginevyo kutumiwa bila ruhusa ya TKM. Tunaomba TKM itajwe kama chanzo cha taarifa na kwamba umiliki au maandishi kuhusu picha vyote vilevile viainishwe kwa mpiga picha au mwandishi au TKM, kama inavyofaa.

Iwapo haki ya kunakili imeashiriwa kwenye picha, mchoro, au nyenzo nyingine yoyote, ruhusa ya kunakili nyenzo hizi lazima zipatikane kutoka kwa chanzo asili. Aidha, inafaa ufahamu kwamba sheria ya jiinai, 18 U.S.C. 713, inakataza matumizi ya Muhuri Mkuu wa Marekani katika hali fulani zilizoainishwa kwenye sehemu hiyo; kwa hivyo tunapendekeza kwamba uwasiliane na wakili kabla ya kutumia Mhuri Mkuu katika muktadha wowote.

Tuzo kwa Mahakama inasimamiwa na Huduma ya Usalama ya Kidiplomasia ya Idara ya Jimbo la Marekani (DSS). DSS inajumuisha sehemu kuhusu Tuzo kwa Mahakama kwenye tovuti yake rasmi: https://www.state.gov/rewards-for-justice/. Ukurasa wa tovuti huo unaunganishwa moja kwa moja na tovuti hii – tovuti rasmi ya RFJ – ya watu kuwasilisha vidokezo.

SUBMIT A TIP

Do Your Part. Secure a Safer World.

There are many ways to submit information to Rewards for Justice.

You may choose from multiple platforms and contact us in numerous languages. To process your information efficiently, we ask you to state your information as succinctly as possible, provide your name, location, and preferred language, and upload all relevant files such as photographs, videos, and documents to support your information. An RFJ representative will soon contact you. Please be patient, as RFJ reads every tip we receive.

Please open your Line app to submit a tip. The number is +1 202 702 7843

Please open your Viber app to submit a tip. The number is +1 202 702 7843

Please visit our Tor-based tips-reporting channel at: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Wasilisha Kidokezi

Fanya Jukumu Lako - Dhamini Ulimwengu Salama Zaidi

Zipo njia nyingi kuwasilisha kidokezo.

Unaweza kuchagua kutoka majukwaa mengi na kuwasiliana nasi katika lugha nyingi.
Kuchakata taarifa yako kwa ufanisi, tunakuomba kusema taarifa zako kwa maneno mafupi na Dhahiri iwezekanavyo, kutoa jina lako, mahali uliko, na lugha unayopendelea, na kupakia faili zote husika kama vile picha, video, na hati kuunga mkono taarifa yako. Mwakilishi wa TKM atawasliana nawe hivi karibuni. Tafadhali uwe na Subira, kwa kuwa TKM husoma kila kidokezo tunachopokea.

Tafadhali fungua programu yako ya Line ili kuwasilisha kidokezo. Nambari hiyo ni +1 202 718 4649

Tafadhali fungua programu yako ya Viber ili kuwasilisha kidokezo. Nambari hiyo ni +1 202 718 4649

Tafadhali tembelea idhaa yetu ya kuripotia vidokezo inayotumia mfumo wa TOR katika: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Skip to content