Tovuti rasmi ya serikali ya Marekani
Kuhusu

Ilani ya Faragha

Ilani ya Faragha

Shukrani kwa kuchagua kuwa sehemu ya jamii yetu ya Tuzo kwa Mahakama. Tunaahidi kulinda taarifa zako za kibinafsi na haki yako ya faragha.

Ilani hii ya faragha inaeleza jinsi tungetumia taarifa zako iwapo:

Katika ilani hii ya faragha, kama tunarejelea:

  • “Tovuti,” tunarejelea tovuti yetu yoyote inayorejelea au kuunganisha na sera hii
  • “Huduma,” tunarejelea tovuti, na huduma zingine husika, pamoja na uuzaji au hafla

Madhumuni ya ilani hii ya faragha ni kukuelezea kwa njia wazi kabisa iwezekanavyo taarifa tunayokusanya, vile tunavyoitumia, na haki ulizonazo kuhusu taarifa hiyo. Iwapo kuna vipengele vyovyote katika ilani hii ya faragha usivyokubaliana navyo, tafadhali sitisha mara moja matumizi ya huduma zetu.

Tafadhali soma ilani hii ya faragha kwa makini, kwa vile itakusaidia kuelewa tunachofanya na taarifa tunazokusanya.

Taarifa Zinazokusanywa Kiotomatiki

Kwa Kifupi Baadhi ya taarifa – kama vile anwani ya Itifaki ya Utambulisho wa kompyuta mtandaoni (yaani IP) na/au sifa bainifu za kivinjari cha mtandao na za kifaa chako – hukusanywa kiotomatiki kila unapotembelea Tovuti yetu.

Tunakusanya kiotomatiki taarifa fulani unapotembelea, tumia, au kuvinjari Tovuti yetu. Taarifa hizi hazifichui utambulisho wako mahususi (kama vile jina lako au maelezo ya kuwasiliana nawe), lakini zinaweza kuwa ni pamoja na taarifa za kifaa na matumizi yake, kama vile anwani yako ya IP, sifa bainifu za kivinjari cha mtandao na kifaa, mfumo endeshi, lugha unazopendelea, viungo rejeleshi vya URL, jina la kifaa, nchi, mahali, taarifa kuhusu jinsi na wakati wewe hutumia Tovuti yetu na taarifa zingine za kiufundi. Taarifa hizi kimsingi zinahitajika kudumisha usalama na uendeshaji wa Tovuti yetu, na kwa ajili ya uchanganuzi wetu wa ndani na kwa madhumuni ya kuripoti.

Kama zifanyavyo biashara nyingi, sisi pia hukusanya taarifa kupitia vidakuzi na teknolojia zinazofanana.

Taarifa tunazokusanya ni pamoja na:

  • Data za Kumbukumbu na Matumizi: Data za kumbukumbu na matumizi ni kuhusu huduma, kwa uchunguzi, taarifa za matumizi na utendaji ambazo huduma zetu hukusanya kiotomatiki unapoingia au kutumia Tovuti yetu na ambazo tunarekodi kwenye faili za kumbukumbu. Kulingana na jinsi unavyowasiliana nasi, hizi data za kumbukumbu zinaweza kuwa ni pamoja na anwani ya IP, taarifa za kifaa, aina na mipangilio ya kivinjari cha tovuti na taarifa kuhusu shughuli zako kwenye Tovuti (kama vile mihuri ya tarehe/saa inayohusiana na matumizi yako, kurasa na faili ulizoangalia, utafutaji na vitendo vingine unavyofanya, kama vile vipengele unavyotumia), taarifa za tukio la kifaa (kama vile shughuli za mfumo, ripoti za makosa (mara nyingine zinazoitwa ‘majaa ya kuvunjika’) na mipangilio ya mitambo.
  • Data za Kifaa: Tunakusanya data za kifaa kama vile taarifa kuhusu kompyuta yako, simu, kompyuta ndogo, au kifaa kingine unachotumia kuingia Tovuti yetu. Kutegemea kifaa kilichotumika, data hizi za kifaa zinaweza kuwa ni pamoja na nambari za kifaa za anwani yako ya IP (au programu andalizi) na za utambulisho wa programu, eneo, aina ya kivinjari cha tovuti, mtindo wa mtambo, na taarifa za mpangilio wa mfumo.
  • Data za eneo: Tunakusanya data za eneo, kama vile taarifa kuhusu eneo la kifaa chako ambayo inaweza kuwa sahihi kabisa au isiyo sahihi kabisa. Kiwango cha taarifa tunazokusanya hutegemea aina na mipangilio ya kifaa unachotumia kuingia Tovuti yetu. Kwa mfano, tunaweza kutumia GPS na teknolojia zingine kukusanya data za eneo kijiografia ambazo zinatuambia eneo ulipo sasa (kulingana na anwani yako ya IP). Unaweza kuchagua kutoturuhusu kukusanya taarifa hizi ama kwa kukataza uwezo kuzifikia taarifa hizi au kwa kuondoa mpangilio wa kuwezesha kujua eneo ulipo kwenye kifaa chako. Kumbuka, hata hivyo, ikichagua kujiondoa, huenda usiweze kutumia vipengele fulani vya hizi Huduma.

Taarifa Zako Tunazitumia Vipi?

Tunatumia taarifa binafsi zilizokusanywa kupitia kwa Tovuti yetu kwa madhumuni mbalimbali ya kibiashara kama ilivyoelezwa hapa chini.

Tunaweza kutumia data zinazokuhusu kwa madhumuni yafuatayo:

  • Kulinda Huduma zetu. Tunaweza kutumia taarifa zako kama sehemu ya jitihada zetu za kudumisha Tovuti yetu salama na thabiti (kwa mfano, kwa minajili ya ufuatiliaji na uzuiaji wa udanganyifu.)
  • Kutekeleza sheria, masharti, na sera zetu kutimiza matakwa ya kisheria na udhibiti.
  • Kukamilisha na kuunga mkono harakati ya sasa
  • Kuendesha na kudumisha Tovuti na mfumo
  • Kufanya utafiti na maendeleo
  • Kufanya uchunguzi wa kisheria ulioidhinishwa

Je, Tunatumia Vidakuzi na Teknolojia Zingine za Kufuatilia?

Kwa Kifupi: Huenda tukatumia vidakuzi na teknolojia za kufuatilia zinazofanana (violeza vya mtandaoni na pikseli) kukusanya au kuhifadhi taarifa.

Vidakuzi na teknolojia zinazofanana zinaweza kutusaidia kiotomatiki kukutambua unaporejea kwenye tovuti au programu yetu. Vidakuzi hutusaidia kuangalia upya mielekeo ya trafiki ya tovuti, huimarisha tovuti, na kuamua ni Huduma gani ni maarufu. Tunaweza pia kutumia taarifa kama hizo kutoa maudhui yaliyobinafsishwa na kutangaza kwa watumiaji wa Huduma ambao tabia zao zinaashiria kwamba wana shauku kwenye mada mahususi.

Vivinjari vingi vya mtandao vimewekwa kwa chaguo-msingi kukubali vidakuzi. Ukipendelea, kwa kawaida unaweza kuchangua kuweka kivinjari chako cha mtandao kuondoa vidakuzi na kukataa vidakuzi. Ukichagua kuondoa vidakuzi au kukataa vidakuzi, hii ingeathiri vipengele au huduma muhimu za Tovuti yetu.

Tunawekaje Taarifa Zako Salama?

Kwa Kifupi: Tunanuia kulinda taarifa zako za kibinafsi kupitia mfumo wa mpango na hatua za kiusalama na kiufundi.

Tumetekeleza hatua za kiusalama na mpango zifaazo ambazo ziliundwa ili kulinda usalama wa taarifa yoyote tunayoshughulikia. Hata hivyo, licha ya hatua zetu za ulinzi na juhudi za kuweka taarifa zako salama, hakuna upitishaji wa kielektroniki kupitia mtandao au teknolojia ya kuweka taarifa ambayo inaweza kulindwa ili kuwa salama kwa asilimia 100, kwa hivyo hatuwezi kuahidi au kuhakikisha kwamba wadukuzi, wahalifu wa mtandaoni, au watu wengine isipokuwa wewe nasi hawataweza kushinda usalama wetu, na kukusanya kwa njia isiyofaa, kufikia, kuiba au kubadilisha taarifa zako. Ingawa tutajaribu kadiri ya uwezo wetu taarifa zako za kibinafsi, upitishaji wa taarifa za kibinafsi hadi na kutoka kwenye tovuti yetu ni kwa hatari yako mwenyewe. Unapaswa tu kuingia kwenye tovuti hiyo katika mazingira salama.

Vidhibiti vya Vipengele vya Usifuatilie

Vivinjari vingi vya mtandao na baadhi ya mifumo ya kuendesha simu na programu tamba hujumuisha kipengele cha Usifuatilie (“DNT”) au mpangilio ambao unaweza kuamilisha ili kuashiria pendeleo lako la faragha ili data kuhusu shughuli zako za kuvinjari mtandaoni isifuatiliwe na kukusanywa. Katika hatua hii, hakuna kiwango sawa cha teknolojia cha kutambua na kutekeleza ishara za DNT ambacho kimekamilishwa. Kwa hivyo, kwa sasa hatushughulikii ishara za kivinjari za DNT au taratibu nyingine ambazo hutoa taarifa moja kwa moja kuhusu chaguo lako la kutofuatiliwa mtandaoni. Ikiwa kiwango cha cha ufuatiliaji wa mtandao kitaidhinishwa ambacho ni lazima tukifuate siku za usoni, tutakujulisha kuhusu shughuli hiyo katika nakala iliyohaririwa upya ya ilani hii ya faragha.

Ilani kwa Watu Wanaoingia Tovuti Hii kutoka Nje ya Marekani

Huduma zetu zinadhibitiwa na kuendeshwa nasi tukiwa Marekani, zinawasilishwa kwa wakazi wa Marekani, na hazinuiwi kutuweka chini ya sheria au mamlaka ya jimbo lolote, nchi, au eneo isipokuwa za Marekani. Taarifa zozote ambazo unatoa kwa kutumia Huduma hizi huenda zikawekwa, kushughulikiwa, kuhamishwa kati ya na kufikiwa kutoka Marekani na nchi nyingine ambazo huenda hazitahakikisha kiwango cha ulinzi wa taarifa za kibinafsi sawa na cha nchi unakoishi. Ikiwa hutaki taarifa zako za kibinafsi ziondoke nchini mwako, tafadhali usitoe taarifa hizo kwa Tuzo kwa Mahakam ana usitumie tovuti yetu. Kwa kutoa taarifa za kibinafsi kwa Tuzo kwa Mahakama, unakubali wazi-wazi kuhamishwa kwa taarifa zako hadi Marekani.

Tuzo kwa Mahakama au watoaji huduma wake huenda pia ikahamisha taarifa zako za kibinafsi kutoka Eneo la Kiuchumi la Uropa (EEA) hadi mataifa mengine, baadhi ya mataifa hayo yakiwa bado hayajaamuliwa na Tume ya Uropa kutoa kiwango cha kutosha cha ulinzi wa data kuambatana na viwango vya EEA. Kwa uhamisho hadi nchi zisizohitaji kiwango cha ulinzi wa data ambacho kinafikia viwango vya EEA, Tuzo kwa Mahakama hutumia taratibu mbalimbali za kisheria ili kulinda taarifa zako za kibinafsi, zikiwamo kanuni za kimikataba na mahakikisho yaliyoandikwa kutoka kwa watoaji huduma.

Tutashughulikia taarifa zako za kibinafsi kuambatana na Sera ya Faragha bila kujali mahali ambapo taarifa zako za kibinafsi zimewekwa au kufikiwa.

Viungo vya Tovuti za Nje

Viungo vya tovuti zilizo nje ya Serikali Kuu ya Marekani au kutumia majina ya kibiashara, kampuni, au shirika ndani ya tovuti ya Tuzo kwa Mahakama ni kwa ajili ya kumrahisishia kazi mtumiaji. Kutumia huko hakumaanishi uidhinishaji au ruhusa rasmi kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani au programu ya Tuzo kwa Mahakama wa tovuti yoyote ya sekta ya kibinafsi, bidhaa, au huduma.

Sheria ya Ulaghai na Matumizi Mabaya ya Kompyuta

Majaribio yasiyoruhusiwa ya kupakia taarifa na/au kubadilishwa kwa taarifa katika tovuti hii yamezuiwa vikali na yanaweza kushtakiwa chini ya Sheria ya Utapeli na Matumizi Mabaya ya Kompyuta ya 1986, 18 U.S.C. § 1030, na kifungu 1001 cha Kichwa 18.

Sera ya Faragha ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje

Unaweza kutazama sera ya faragha ya tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani katika: https://www.state.gov/privacy-policy/

Jinsi ya Kuwasiliana Nasi

Tunakaribisha mrejesho ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera yetu ya faradha au matumizi ya taarifa yako.
Nyenzo za Wizara za kufuata faragha zinapatikana kwenye Tathmini za Athari za Faragha (PIA) na Ilani za Mifumo ya Rekodi (SORN). Kwa taarifa zaidi kuhusu Sera yetu ya Faragha, tafadhali wasiliana nasi katika privacy@state.gov au utuandikie baruapepe katika:

Office of Global Information Services
Privacy Office – A/GIS/PRV
State Annex 9
U.S. Department of State
Washington, DC 20006

SUBMIT A TIP

Do Your Part. Secure a Safer World.

There are many ways to submit information to Rewards for Justice.

You may choose from multiple platforms and contact us in numerous languages. To process your information efficiently, we ask you to state your information as succinctly as possible, provide your name, location, and preferred language, and upload all relevant files such as photographs, videos, and documents to support your information. An RFJ representative will soon contact you. Please be patient, as RFJ reads every tip we receive.

Please visit our Tor-based tips-reporting channel at: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Wasilisha Kidokezi

Fanya Jukumu Lako - Dhamini Ulimwengu Salama Zaidi

Zipo njia nyingi kuwasilisha kidokezo.

Unaweza kuchagua kutoka majukwaa mengi na kuwasiliana nasi katika lugha nyingi.
Kuchakata taarifa yako kwa ufanisi, tunakuomba kusema taarifa zako kwa maneno mafupi na Dhahiri iwezekanavyo, kutoa jina lako, mahali uliko, na lugha unayopendelea, na kupakia faili zote husika kama vile picha, video, na hati kuunga mkono taarifa yako. Mwakilishi wa TKM atawasliana nawe hivi karibuni. Tafadhali uwe na Subira, kwa kuwa TKM husoma kila kidokezo tunachopokea.

Tafadhali tembelea idhaa yetu ya kuripotia vidokezo inayotumia mfumo wa TOR katika: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Skip to content